JE TETENASI NI NINI?
UJUE UGONJWA WA TETENASI (TETANUS).
Tetenasi (tetanus) ni ugonjwa unaotokea sana maeneo ya AFRICA na kuathiri idadi kubwa ya watu, na unasababishwa na
Bacteria anaejulikana kwa jina la Clostridium tetani anaepatikana
ardhini (kwenye mchanga au udongo), na kwenye vinyesi vya wanyama na
binadamu.
Kwa kawaida hawa bacteria
wanaosababisha Tetenasi wanaishi katika utumbo mdogo wa binadamu au wanyama na
wanatoka ndani ya mwili wa binadamu au mnyama aliye athirika pamoja na kinyesi
kisha wanatengeneza vijimbegu (spores) ambavyo vinaweza kustahimili mazingira
ya nje.
Ugonjwa wa tetenasi
unaweza kumpata mtu pale ambapo huyu bacteria (Clostridium tetani) ameingika
katika mwili wa binadamu kupitia kwenye kidonda kilichopo katika sehemu yeyote ya mwili wake.
Hizi ni aina za vidonda
ambavyo bacteria wa tetenasi anaweza kuingia:-
1. Kidonda
ambacho hakipo katika hali ya usafi.
2. Kidonda
kilicho chimbika sana.
3. Kidonda
kilichotokana na moto (kuungua) chenye mzunguko wa damu chache.
4. Kidonda
kilichotokana na Upasuaji uliofanywa navifaa ambanyo siyo salama (havikuoshwa
vizuri na kutunzwa mbali na mazingira ambayo bacteria wanaweza kukaa na
kuzaliana)
5. Kidonda
kilichotokana na mtu kujikata na kitu chenye ncha kali kama vile Bati,
kujichoma na Msumali au kuumia kutokana na ajari ya Gari, Pikipki n.k.
6. Kwa
watoto wachanga katika kitovu kilichokatwa ambacho bado hakijapona na pia vifaa
ambavyo siyo salama vilivyotumika kukata kitovu.
7. Kwa
mwanamke aliyetoa mimba au kujifungua kwa kutumia vifaa ambavyo sio salama
8. Kidonda
kinachotoa usaa au majimaji.
DALILI
ZA UGONJWA WA TETENASI
Zifuatazo ni dalili ambazo zitamtokea mtu ambae
tayari ameisha athirika na ugonjwa wa Tetenasi:-
1. Misuli
ya taya kukakamaa na kupelekea mtu kushindwa kufumbua mdomo.
2. Kisha
misuli ya mwili mzima kukakamaa.
3. Maumivu
mwili mzima.
4. Kumeza
chakula n.k kwa shida au kushindwa kumeza kabisa.
5. Kupumua
kwa shida.
6. Kwa
watoto wachanga dalili ya kwanza ni mabadiliko ya ghafla ya hali ya mtoto
aliyekua anaendelea vizuri, kisha ikifuatiwa na dalili hizo hapo juu.
JINSI YA KUJIKINGA NA
UGONJWA WA TETENASI
Yafuatayo
ni mambo ambayo ukiyazingatia utaweza kuepuka kukubwa na ugonjwa wa Tetenasi wewe, familia yako,
na jamii kwa ujumla:-
1. Kufanya
upasuaji mzuri wa kidonda ili kuondoa uchafu ndani ya kidonda.(hii inafanywa na
mtaalamu wa Afya)
2. Kupata
chanjo ya Tetenasi ili kuzuia ugonjwa tetenasi isiweze kutokea.(Hii ni muhumu
sana)
3. Kwa
akina Mama wajawazito kuhakikisha anajifungua katika Hospitali au Kituo cha
afya chini ya uangalizi wa wataalamu wa Afya.
4. Kwa
Wanawake wanao toa mimba kuhakikisha anatoa mimba yake Hospitali au kituo cha
Afya chini ya uangalizi wa wataalamu wa Afya.
5. Kuvaa
vifaa vinavyoweza kukukinga kuumia uwapo katika kazi yeyote inayoweza
kusababisha mtu kuumia kwa namna yeyote ile.
6. Kuhakikisha
umevaa viatu unapokua unatembea, au kusimama juu ya ardhi. (usikanyage ardhi
bila viatu miguuni)
7. Kama
una kidonda sehemu yeyote ya kuhakikisha kinakuwa katika hali ya usafi na ukavu
mda wote.
N.B:-
Ugonjwa wa tetenasi ni hatari sana Duniani kwani ni ugonjwa ambao unaweza
kusababisha kifo kwa mgonjwa ndani ya mda mfupi na pia hakuna kipimo maalumu
cha kupimia ugonjwa huu hivyo ukiona dalili ni vizuri ukiwahi mapema Hospitali
uonane na mtaalamu uweze kupata tiba mapema uweze kuiokoa Afya yako.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteJe!?... sindano ya tetenasi inaleta homa?
ReplyDelete