SAYANSI YA MAPENZI; JE, MAPENZI YANATOKEA VIPI KISAYANSI?!
Professor Arthur Arun amekua akitafitikwanini watu huzama katika mapenzi, akachukua baadhi ya watu na kuwaambia wafanye vitu vitatu(3) ambavyo vimeorodheshwa hapo chini, na kugundua kwamba baada ya kufanya vitu hivyo, hawa watu wawiliwawili (me na ke) walijikuta wakizama katika hisia kali za mapenzi Ghafla!! na siku chache baadae, wawili kati yao walifunga ndoa!!
Na vitu hivyo ni:-
-Tafuta mtu mgeni kabisa maishani mwako
-Kila mtu amsimulie mwenzake kifupi juu ya maisha yake kwa muda wa nusu saa
-kisha tizamaneni machoni bila kuongea kwa muda wa dakika 4.
Unajua ni kwanini “unamzimikia” mtu na kujitoa kwa chochote kwa ajili yake??!
Twende pamoja….
Hali hii inaendeshwa na kemikali mbalimbali katika ubongo zisizoweza kuzuilika (homoni/hormones). Hua tunafikiria kua tunachagua wapenzi kwa maamuzi yetu, lakini kiukweli kemikali hizi zinafanya nafasi kubwa sana katika swala hili, kama tunavyoenda kuona.
Wanasaikolojia wanasemaje?
Wanasaikolojia wanasema inachukua muda wa sekunde 90 hadi dakika 4 ili kuamua kama “umemzimikia” mtu flani, lakini utafiti unaonesha kua hicho kitu kina nafasi ndogo sana, na kuongeza kua kuvutiwa na kufikia kumzimikia mtu kunatokana na:-
l 55% Mvuto wa Muonekano na umbile lake
l 38% Sauti anayoitumia wakati mkiwasiliana
l 7% Tu ndio nafasi ya muda kama wanavyosema wanasaikolojia.
TUNAENDELEAA…
HATUA 3 ZA MAPENZI
Helen Fisher wa Chuo Kikuu cha Rutgers, alipendekeza hatua 3 ambazo hupitiwa na watu katika mapenzi, nazo ni Anasa, Mvuto pamoja na Muunganiko/Mshikamano, na kila moja inaendeshwa na Homoni mbalimbali kama inavyoelezewa;
HATUA YA 1: ANASA
Hii ndio hatua ya kwanza kabisa kuelekea kuzama katika mapenzi, inayo changiwa na homoni ziitwazo Testosterone na Oestrogen kwa wanaume na wanawake, zinazompelekea mtu ajiskie hamu ya kufanya ngono.
HATUA YA 2: MVUTO
Katika hatua hii ndipo unajiskia kuanza kuzama katika mapenzi na mtu flani, hata kabla hamjaongea, na kisayansi inaonekana kwamba hali hii inachangiwa na “Neurotransmitter” (kemikali zinazotumika katika ubongo kuvusha taarifa kutika neva moja hadi nyingine) za aina tatu, ambazo ni adrenaline, dopamine and serotonin, zinachokifanya ni hiki:-
Adrenaline
Mwanzoni mtu anapozama katika mapenzi, kiwango cha adrenaline na cortisol huongezeka kwenye damu, hii humfanya mtu, hata kama alikua katika hali ya kukasirika, awe mchangamfu na mcheshi mara tu anapokutana na mpenzi mpya, ndipo mtu anaanza kutokwa ni kijasho chembamba, mapigo ya moyo huongezeka pia.
(Adrenaline pia ndiyo homoni inayomfanya mtu apate nguvu ghafla anapo kutana na hatari, inayomuwezesha hata akwee mti wenye miiba bila ata kuhisi maumivu!!)
Dopamine
Kemikali hii kutoka katika ubongo humfanya mtu awe kama mtumiaji wa mihadarati aina ya kokein(cocaine). Helen Fisher alifanya uchunguzi wa ubongo wa watu ambao ni wapya na wamezama zaidi katika mapenzi, na akagundua wana kiwango kikubwa cha dopamine.
Dopamine humfanya mtu awe na msisimko wa burudani ya hali ya juu, kujihisi ana nguvu nyingi, asiwe na hamu ya kula wala kulala akiwa na mpenzi wake, na kumkosa mpenzi hata kwa muda kidogo humfanya mtu ahisi kama ana “arosto”.
(kama umewahi kuwa katika penzi zito unaweza ukalithibitisha hili)
Serotonin
Na hatimaye serotonin, kemikali muhimu sana kwa wapenzi, hii humfanya mtu awe anamfikiria mpenzi wake mpya kila wakati, hawezi akakaa dakika chache bila kumtumia sms au hata kumpigia simu walau askie sauti yake.
Katika hatua hii, ndipo watu huwasikiliza zaidi, kuwajali sana na kujitolea kwa chochote kwa ajili ya wapenzi wao kuliko hata wazazi wao na ndugu wengine ambao wanaweza wakawa wa msingi zaidi kuliko hata huyo mpenzi.
HATUA YA TATU: MUNGANIKO/MSHIKAMANO
Hapa, wapenzi wanakua na bond inayowawezesha kushikamana kwa muda mrefu hata kufikia uamuzi wa kupata na kukuza watoto. Kisayansi, hali hii inaonekana kuchangiwa na homoni tatu, Oxytocin pamoja na Vasopressin, Kivipi??
Oxytocin
Hii ni homoni yenye nguvu ambayo hutolewa na wanawake na wanaume wakati wa kufikia kilele wanapofanya ngono.
Hii huzidisha zaidi ile hali ya kujiskia karibu zaidi na mtu baada ya kufanya nae mapenzi, na ipo hivi, kadri unavyofanya mapenzi na mtu mara nyingi, ndivyo ukaribu wenu na mahusiano yanazidi kuwa na nguvu zaidi.
Oxytocin pia ndiyo inayo zidisha zaidi upendo wa mama kwa mtoto, na hutolewa wakati wa kuzaliwa, pia humsisimua mama aweze kutoa maziwa pale tu anapo muona au hata kuskia sauti ya mtoto wake mchanga.
Diane Witt, Professor kutoka New York, alionesha kwamba ukikwamisha utoaji wa kawaida wa homoni hii kwa kondoo na panya, hua wanawakataa watoto wao!!
Vilevile, kinyume chake, kama ukiiweka kwa majike ya panya ambayo hayajawahi kupandwa, panya hao huanza kujipendekeza kwa watoto wa panya wengine na kuwafanya kama watoto wao.
Vasopressin
Hii pia ni muhimu na hua pia inatolewa baada ya kufanya ngono, jina jingine inajulikana kama Anti-diuretic-hormone ambayo mara nyingi husaidia kusawazisha concentation ya chumvi na maji katika damu.
Walipo ifanyia utafiti kwa wanyama iligundulika kuwa, wakiondolewa homoni hii huachana, na kutowajali wapenzi wao.
Kwaiyo, usije ukashangaa mtu akazama katika mapenzi na akashindwa hata kufanya vitu vya msingi na kuishia kutumia muda na mali zake kwa mpenzi wake.
Share na wenzako katika Facebook, Whatsapp na Linkedin waweze kusoma, pia tuandikie maoni yako katika eneo la Comment, karibu tena.
No comments